Wazo la Leo : Je unayo Furaha, Je furaha yako ipo wapi ?. Unafanyaje kuipata ?

Hakuna mtu asiyependa kuwa na furaha , ambaye yeye anapenda tu huzuni na maumivu. mimi binafsi napenda furaha na amani pia, sijui wewe msomaji wangu.

wakati namaliza mwaka nimejifunza meengi kuhusu furaha yangu, kupitia mambo meengi na changamoto nikajua vile ambavyo sipaswi kufanya kwaajili ya furaha yangu.

Ukitaka Furaha huwezi kuikosa, kama utaamua. kumbuka pia kuwa Furaha inatafutwa haiji peke yake, kumbe kuna jitihada katika hilo. Unaweza kutengeneza kupitia wewe mwenyewe lakini pia kuptia wengine

Mpenyoo.jpg

Juzi hapa nilikutana na hii :
” furaha ni kitu unachokitengeneza baada ya kuwa umewezeshwa, lakini uwezesho unatafutwa,…. ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. Yohana 16:23, 24. Kama huna furaha maana yake hujapewa, na kama hujapewa Hujaomba. Na wanufaika wa maombi si wewe peke yako, hata Mungu anafaidika, kwa kutukuzwa na anapenda kutukuzwa. Sasa anawezaje kukunyima kama naye ni mfaidika…..
Unapoomba kitu Mungu anakupa ili kwanza ufaidike wewe na pili afaidike yeye- kwa kutukuzwa na watu.
Si lazima saaana uwaambie na kuwalazimisha watu kwa nguvu zako wamtukuze Mungu wako, lakini Mungu akikujibu watalazimika kumtukuza.

Matokeo ya Maombi yako yalazimishe wamtukuze na kumwabudu Mungu”

usiache kuitengeneza furaha yako, hakuna mtu ataleta kama hujatengeneza, na usitegemee sana furaha ya mtu mwingine

mimi nimeamua sasa ,hakuna mtu ataharibu furaha yangu na kutangaza na kusambaza huzuni kwangu ati kwa vile namtegemea anifurahishe, natengeneza na kutafuta halafuuuu…itajileta ya kunitooshaaa. Pia nimeamua kutomnyima mtu furaha anayostahili, njooo uchukue,.

Advertisements