Maisha Na Mahusiano : Maisha Mazuri Yanajengwa Na Mahusiano Bora

Sam n Friends (2).jpg

Tunaweza  kujifunza mambo matatu kutoka katika Mahusiano.

La kwanza Ni kuwa, Muunganiko wa kijamii ni kitu kizuri kwa Mwanadamu na Upekee Unaua. Hivyo, watu wenye Mwunganisho/uhusiano mkubwa na jamii zao, familia zao, na marafiki zao,na huwa wenye furaha zaidi, na huwa na Afya njema ya Mwili, na wanaishi muda mrefu kuliko watu wale walio na uhusiano mdogo.  Na Uzoefu wa upweke hugeuka kuwa Sumu.. watu waliotengwa sana na wanaotaka kuwa mbali na watu hujikuta hawana furaha ya kutosha, Afya zao hushuka mapema katika umri wa Kati, Utendaji kazi wa ubongo huzorota mapema na huishi maisha mafupi zaidi  ya watu wasio Wapweke. Na ukweli wa Kuhuzunisha ni kuwa ,zaidi ya Mmarekani mmoja Kati ya watano Hupatikana akiwa Mpweke.

Tunajua unaweza kuwa Mpweke katika kundi na unaweza kuwa Mpweke katika Ndoa, hivyo funzo kuu la pili tujifunzalo ni kuwa “ si idadi ya Marafiki ulionao,na si kuwa au kutokuwa katika Mahusiano thabiti, bali ni Ubora wa mahusiano yako ya Karibu ndiyo kitu cha kuzingatia’’ .. kuishi kati ya dimbwi la migogoro ni mbaya sana kwa Afya zetu. Ndoa zenye migogoro mikubwa , kwa mfano, Zisizo na Huba/Upendo mwingi, hugeuka kuwa hatari kwa Afya zetu zaidi hata ya kupata Taraka. Na kuishi katika Dimbwi la Mahusiano motomoto, mazuri ni Ulinzi na Usalama.

happiness.jpg

Na funzo kubwa la tatu tunalojifunza kuhusu mahusiano na Afya zetu ni kuwa, Mahusiano bora hayalindi miili yetu pekee, pia yanalinda Akili zetu. Inageuka kuwa, ukiwa katika mahusiano thabiti na watu wengine, uzee wako utakuwa salama., kwamba watu walio katika mahusiano ambayo wanahisi kabisa wanaweza kuwatazamia wengine katika vipindi vya Uhitaji, ni watu wenye kuwa na kumbukumbu ya haraka inayodumu kwa muda mrefu. Na watu wale walio katika mahusiano ambayo wanahisi hawawezi kuwahusisha na kuwatazamia wengine ,hawa ni wale ambao hupata kupoteza kumbukumbu mapema zaidi.

Na yale Mahusiano mazuri , si kwamba hutakiwa kuwa Shwari wakati woote. Kuna wakati wanagombanagombana na kubishanabishana siku nzima, lakini kila wanapohisi kwamba watahitajiana , mabishano hayo hayaweki huzuni katika kumbukumbu zao.

Hivyo ujumbe huu, kwamba Mahusiano bora Na ya Karibu Ni bora kwa afya zetu na Maendeleo yetu, hii ni Hekima kongwe kama Vilima.  Kwanini hii ni ngumu kupata na Rahisi kupuuzia ? kwasababu sisi sote ni wanadamu . tunachoweza kupenda zaidi ni utatuzi wa haraka. Mahusiano yana fujo na yanachanganya, lakini pia ni kitu endelevu kisichoisha . Wengi huamini kwamba kupata umaarufu na utajiri na mafanikio makubwa hupelekea maisha Bora. Lakini mara nyingi uchunguzi uliochukua takribani miaka 75 unaonesha kuwa, Watu waliofanikiwa/waliofika mbali zaidi ni wale walio Egama katika Mahusiano na Familia,Marafiki na Jamii.

Advertisements