Sometimes i am Missing you Mom…

dadaake.jpg

Kuna wakati nakukumbuka saana mama

Waswahili husemaaa...Ajali hubeba ahadi ya Mwenye Tahadhari, je unatumiaje ulichonacho sasa, maana kuna nyakati zaja ambazo hutapata tena ulichonacho.
Wazazi ni Tunu kuu na Ya Pekee. Mwenzako akinyolewa zako tia maji

Najaribu kufikiri huku Machozi yakinitiririka, siku ile ningekwambia: “….Mama nimemaliza darasa la sabaa…” huenda ungenikumbatia na kunibusu paji la uso. Ningefurahi mama, hadi moyoni, hiyo tu ingenitia nguvu

Pia nawaza huenda haupo ili nijue vile ulivyo muhimu, vile ambavyo wengine wanakosa na kumaanisha pale wanapokukosa. na vile ambavyo ningepata nikiwa nawe

Nawaza vile ungenipeleka kununua kiatu na mahitaji ya sekondari, ningefurahi na kukusumbusumbua kwa kufanya machagulio
Lakini vipi siku natakiwa kwenda kusoma mbali shule ya upili, ungeninunulia tranka Mama, na begi,na sare mpya….

Mama , vipi juzi ningekupigia simu na kukwambia nimepata shahada yangu ya kwanza..Mama , nawaza vile ungefurahi,na kushangiliaa na kumshukuru Mungu..ungefurahi mama…
…Kama Yeye Alifurahi saaana na tukafurahi pamoja, Ahsante kwa kuniachia Mwanamke Huyu wa Nguvu,Jasiri na Mpambanaji,..Asiyekata tamaa, Agness Samson, Mama alifurahi, na kushangilia, na mara nyingi alimshukuru Mungu Kwa Hatua Zangu, Tangu Shule ya Msingi hata Chuo Kikuu
..Alinisindikiza Stand na kunipungia mkono,akinitakia safari njema,na mafanikio mema lakini alinipokea niliporudi,.

Mama.. huyu ni Mzazi na amenilea sana na kunifundisha kuishi, Alikuwa Baba kwangu Pia. Mambo mengi ninayoishia leo nimejifunza kwake,yananisaidia. alinifunisha kuishi na watu mbalimbali, ninaowajua na nisiwajua, kuwa na bidii na kujituma. Mama, huyu hakuwahi kukata tamaa, Hili nitashika hadi Mwisho. Hakuna kukata tamaa wala kurudi nyuma. Na yeye namkumbusha…hakuna kukata tamaa, hakuna kurudi nyuma daima Dada 

Mama , uliniacha katika mikono salama na imara hasaaa,
..nilijua umuhimu wako pale nilipokukosa, na yale ningepata  ungekuwepo, maana kuna wengine hawajui, maana hawajakutwa bado
..Mama huku kuna misemo, ati huwezi kujua uzuri au umuhimu wa kitu hadi pale unapokikosa..na nadha huwezi kukumbuka kitu ulichonacho .. hii ni kweli kabisa~ I really missed you Mother Dada.jpg

Mama unajua kuwa Rafiki zake wamekuwa wangu, nimepata ndugu wengi tena maeneo ya mbali, wamekuwa msaada kwangu na nimepata mengi na vingi kupitia yeye na wao, najiskia vizuri kwaajili yake. Nimejifunza Mengi, Mi namshukuru Mungu kwaajili yake lakini namumbea zaiidiiiii. Nnavosema haya bado yupo namimi bega kwa bega,hajaniacha

Mama kila nikikukumbuka Sura ya Mwanamke huyu Jasiri hunijia, Matendo yake kwangu yakipita fikrani baada ya machozi napata tabasamu. Mimi nimekuwa Kifungua Mimba wake,First Born wake..lakini huyu ni Dada, Ndugu,Rafiki na Mtani Kwangu, Amekuwa sababu kwangu. Mama Sasa ana watoto wazuri sana Kama Yeye na Wote Majina yao Mazuri na Yanaanza Na B…Blandina na Blessed Tuko Tripple B

Mama Ahsante Kwa Kuniachia Huyu, Shujaa na Malkia wa Nguvuu,

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s